Hoppa till innehållet

Jinsi Kivra inavyofanya kazi

Katika Kivra unapokea karatasi muhimu. Kwa mfano, ankara, risiti na barua kutoka kwa makampuni na mamlaka.

Så funkar kivra

Kivra ni nini?

What is Kivra

Pokea na uhifadhi

Kivra ni zana tumizi (App) ambayo unaweza kutumia kupokea na kuhifadhi karatasi muhimu. Unaweza pia kupakia hati kwa Kivra.

Soma barua zako popote duniani

Unaweza kufikia kila kitu katika Kivra kwenye kompyuta au simu ya mkononi, mahali popote na wakati wowote. Kwa kuwa Kivra ni huduma ya kidijitali, anwani yako ya mahali ulipo haijalishi. Ukihama, haitaathiri Kivra yako.

Mambo hayo unaweza kupokea katika Kivra

Barua ya kidigitali

Unapokea barua kidijitali kutoka kwa makampuni na mamlaka, kama vile Skatteverket (Mamlaka ya kodi na ushuru) na Försäkringskassan (Wakala wa bima ya kijamii).

Risiti ya kidigitali

Unapokea risiti katika zana tumizi (App) yako badala ya risiti za karatasi dukani.

Ankara za kidigitali

Unaweza kulipa ankara (bili) moja kwa moja huko Kivra.

Taarifa ya mshahara ya kidigitali

Ikiwa mwajiri wako anatumia Kivra, utapokea taarifa ya mshahara katika zana tumizi (App).

Vipakiwa

Unaweza kupakia karatasi kwa Kivra. Hivyo zitahifadhiwa kidijitali.

Jisikie salama ukiwa na Kivra

Viktigt ID-säkerhet – img

Kivra ni salama

Usalama ni muhimu kwetu. Ni wewe pekee unayeweza kufikia vitu vyako katika Kivra. Unaingia kwa kutumia Kitambulisho cha Benki ya Simu (Mobile BankID). Unaweza kuwaamini watumaji wote huko Kivra. Sisi hatusomi mambo yako. Kila kitu kinachotumwa husimbwa kwa njia fiche na kuhifadhiwa katika vituo vya data vya Uswidi.

Ni rahisi kufuatilia mambo yako katika Kivra

Tunarahisisha kukumbuka barua na ankara. Mara tu utakapopokea kitu kipya huko Kivra, tutakutumia barua pepe. Pia tutakutumia kikumbusha kwa barua pepe kuhusu barua ambazo hazijasomwa na ambazo hazijashughulikiwa. Kumbuka kupakua zana tumizi yetu na kuwasha arifa. Hivyo utajua mara moja wakati kitu kipya kimetua Kivra.

Jinsi ya kupata Kivra

Ili kupata Kivra, lazima kwanza uwe na Nambari ya utambulisho binafsi ya Uswidi na Kitambulisho cha Benki ya Simu (Mobile BankID). Kisha bonyeza kitufe na ufuate maagizo. Inaenda haraka.
Läs mer villkor

Masharti yetu ya matumizi

Unapopata Kivra, barua pepe zitaanza kutumwa kwako kidijitali katika zana tumizi. Baadhi ya makampuni hayatumi kupitia Kivra. Kutoka kwao, unaweza kupokea barua ya karatasi kwenye sanduku lako la barua. Unaweza kuchagua ni nani unayetaka akutumie barua kwa Kivra. Unafanya hivi katika mipangilio. Soma masharti yetu ya matumizi hapa.

Wasiliana nasi

Una maswali? Karibu utumie mawasiliano nasi.